Barcelona Yapambana Kumpa Rashford Mkataba wa Kudumu

Klabu ya Barcelona inaendelea kufanya juhudi kubwa za kuhakikisha inamnasa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, kwa mkataba wa kudumu baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha akiwa kwa mkopo msimu uliopita.

Barcelona Yapambana Kumpa Rashford Mkataba wa KudumuKwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka Ulaya, Rais wa Barcelona, Joan Laporta, anaongoza harakati za kukamilisha usajili huo licha ya ushindani mkali kutoka klabu kadhaa za Ligi Kuu England na Bundesliga.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Barcelona wanaamini Rashford ni mchezaji anayefaa katika mradi wao wa muda mrefu na wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha anabaki Camp Nou,” zimeeleza taarifa zinazofuatilia mazungumzo hayo.

Barcelona Yapambana Kumpa Rashford Mkataba wa KudumuHata hivyo, Barcelona wanakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich, Newcastle United, Tottenham Hotspur na Aston Villa, ambazo zote zimeonyesha nia ya kupata saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 28.

Barcelona Yapambana Kumpa Rashford Mkataba wa KudumuRashford aling’ara akiwa Barcelona msimu uliopita baada ya kufunga mabao 14 na kutoa pasi 14 za mabao, mchango uliosaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa La Liga. “Mafanikio yake nchini Hispania yameifanya Barcelona kuona umuhimu wa kuendelea kuwa naye kwa muda mrefu,” vyanzo vya karibu na klabu hiyo vimeeleza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.