Taarifa za ndani zinaeleza kiungo wa klabu ya Real Madrid Jude Bellingham anatajwa kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana chini ya miaka 21(Golden Boy)inayotarajiwa kutolewa kesho.

Kiungo Bellingham anaingia kuwania tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo ambapo mwaka jana alikosa tuzo hiyo mbele ya kiungo wa klabu ya Barcelona Gavi, Lakini vyanzo vinaeleza kua mshindi wa tuzo hiyo awamu hii ni kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza.bellinghamKiungo huyo fundi amekua na mwaka mzuri sana tangu akiwa na Borussia Dortmund na wakati huu akiendelea kuuwasha moto ndani ya klabu ya Real Madrid mabingwa wa muda wote barani ulaya.

Taarifa ya Jude kushinda tuzo hiyo ambayo inatolewa kesho imevuja kama ambavyo taarifa zimevuja kua Lionel Messi anatarajiwa kushinda tuzo yake ya nane ya Ballon Dor hapo kesho.bellinghamKutokana na ubora mkubwa ambao ameuonesha Bellingham ndani ya klabu ya Real Madrid ni wazi mchezaji huyo anastahili tuzo hiyo, Lakini pia magoli mawili aliyofunga kwenye El Clasico jana siku mbili kabla ya tuzo yanaendelea kuchochea kuipata tuzo hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa