Bellingham: Sijafata Pesa Real Madrid

Kiungo mpya wa klabu ya Real Madrid ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Borussia Dortmund Jude Bellingham amesema hajajiunga na klabu hiyo kwasababu ya pesa.

Kiungo Bellingham amesema hayo wakati wa utambulisho wake rasmi leo akisema kua kujiunga na klabu ya Real Madrid haikua suala la pesa kwani klabu hiyo ni klabu kubwa kabisa ulimwenguni na ndio sababu ya kiungo kujiunga na wababe hao wa soka duniani.BellinghamKiungo huyo ameweka wazi kua sababu kubwa iliyomfanya kujiunga na klabu ya Real Madrid ni pale alipohudhuria mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool ambapo Real walishinda kwa bao moja kwa bila na ndipo alipoona kujiunga na Madrid ni uamuzi sahihi kwake.

Jude Bellingham amejiunga na klabu ya Real Madrid kama mchezaji ghali kabisa msimu huu kwenye kikosi cha klabu hiyo na kwake amesema kujiunga na klabu hiyo ni kama ndoto kutimia kwake kwani klabu hiyo ni ndoto ya wachezaji wengi duniani.BellinghamKiungo Bellingham atavaa jezi namba tano ambayo ni jezi yenye heshima sana klabuni hapo kwani imevaliwa na magwiji mbalimbali na mmoja wao ni Zinedine Zidane ambaye kwa Jude ni kama kioo kwake na wengi wanaamini mchezaji huyo ataitendea haki jezi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.