Bellingham Mchezaji Bora wa Wiki La Liga

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza Jude Bellingham amefanikiwa kua mchezaji bora wa wiki wa ligi kuu nchini Hispania La liga.

Kiungo Jude Bellingham amefanikiwa kua mchezaji bora wa wiki kutokana na alama alizokusanya katika mchezo wao wa wikiendi hii na kufanikiwa kuongoza akiwa na jumla ya alama 9.4 akiwashinda wachezaji wote waliocheza wikiendi iliyomalizika.BellinghamKiungo huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alifanikiwa kufunga mabao mawili kwenye wikiendi iliyomalizika ambapo klabu yake ya Real Madrid ilifanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.

Kiungo huyo mpaka sasa ana mabao matatu katika michezo miwili ya ligi kuu ya Hispania ambayo ameitumikia klabu ya Real Madrid, Lakini pia anaongoza kwenye orodha ya wafungaji bora mpaka sasa akiwa na mabao yake matatu.BellinghamMwanzo wa kiungo Jude Bellingham ndani ya klabu ya Real Madrid umekua mzuri kwa mchezaji huyo na klabu hiyo, Huku watu wengi wakimtabiria makubwa mchezaji huyo kutokana na mwanzo wake ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe