Kiungo wa kimataifa Uingereza Jude Bellingham anayekipiga ndani ya klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ameweka wazi kua anatamani kukipiga ndani ya klabu hiyo kwa miaka 10-15 mbele.
Kiungo Bellingham ameonesha kua anataka kukaa ndani ya Real Madrid kwa muda mrefu na kufanya mambo makubwa zaidi, Kwani mpaka sasa mchezaji huyo ameanza vizuri ndani ya timu hiyo.Kiungo huyo baada ya mchezo wa timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Italia ambapo walishinda kwa mabao matatu kwa moja aliweka wazi kua ana furaha kubwa kucheza ndani ya klabu ya Real Madrid, Lakini pia akiweka wazi kua kuwepo ndani ya timu hiyo kunamjenga kwa kiwango kikubwa kutokana ubora wa wachezaji waliopo klabuni hapo.
Kiungo huyo amekua na mwanzo mzuri sana ndani ya Real Madrid kwani mpaka sasa ameshafanikiwa kufunga mabao 10 katika michezo 10 ambayo ameichezea klabu hiyo mpaka sasa, Lakini pia akisaidia upatikanaji wa mabao matatu kwa kupiga pasi za mwisho.Kiungo Jude Bellingham pia ameweka wazi kufurahishwa na kocha wa klabu hiyo namna anampa uhuru wa kuonesha ubora wake ndani ya klabu hiyo, Kocha Ancelotti ameonesha kumpa uhuru mkubwa kiungo huyo na ndio sababu ya kuonesha ubora mkubwa.