Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza Jude Bellingham atakuepo kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya klabu ya Barcelona siku ya Jumamosi.

Jude Bellingham ilifahamika kua amepata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Sporting Braga, Lakini taarifa inaeleza kua kiungo huyo hakupata majeraha makubwa na atakuepo kwenye El Clasico.bellinghamKiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza leo ameonekana kwenye video fupi akieleza mwenywe kua atakuepo kwenye mchezo kati ya klabu yake dhidi ya Barcelona siku ya jumamosi baada ya uvumi kua hatakuepo kwenye mchezo huo.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua kwenye kiwango bora sana tangu atue klabuni hapo majira ya joto, Taarifa yake ya kupata majeraha na kuelezwa huenda akaukosa mchezo dhidi ya Bracelona uliwashtua mashabiki wa klabu hiyo.bellinghamJude Bellingham ameshafanikiwa kufunga mabao 11 kwenye michezo 12 ambayo ameshacheza mpaka sasa hivi ndani ya klabu hiyo, Huku akifanikiwa kupiga pasi tatu za mabao na kumfanya kuhusika na mabao 15 klabuni hapo mpaka sasa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa