Bellingham Kutambulishwa Kesho

Kiungo mpya wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham ambaye alikua anakipiga klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani atatambulishwa kesho mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.

Bellingham ambaye amenunuliwa kwa gharama kubwa ndani ya klabu ya Real Madrid akitokea Borussia Dortmund atatambulishwa kesho mbele ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya leo kutangazwa rasmi kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.BellinghamKiungo huyo ambaye amekua kwenye kiwango kikubwa sana ndani ya klabu ya Dortmund kwa miaka mitatu ambayo ameitumikia klabu hiyo, Huku akitua ndani ya viunga vya Bernabeu kama mchezaji mwenye gharama zaidi.

Klabu ya Real Madrid imelipa kiasi cha Euro milioni 100 kwa kijana huyo mwenye miaka 19 tu lakini yote imeletwa kutokana na ubora ambao Bellingham ameuonesha ndani ya viunga vya Signal Iduna Park kwa miaka ambayo ameitumikia klabu hiyo kongwe nchini Ujerumani.BellinghamJude Bellingham anakua muingereza wa kwanza kuitumikia klabu hiyo baada ya miaka mingi kupita bila raia wa kimataifa wa Uingereza kuitumikia klabu hiyo kubwa kabisa ulimwenguni,Huku mchezaji wa mwisho wa Kiiingereza kuvaa jezi ya Real Madrid alikua David Beckham.

Acha ujumbe