Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema inaelezwa kua yuko kwenye hatihati ya kutimka ndani ya timu hiyo kipindi cha majira ya joto ya usajili.
Vyanzo mbalimbali kutoka nchini Hispania vinaeleza Benzema anawindwa na vilabu mbalimbali kutoka Urabuni ambavyo vimemuekea dau nono mshambuliaji huyo, Hivo inawezekana kwenye dirisha hili kubwa akaondoka ndani ya viunga vya Madrid na kutimkia zake Uarabuni.
Klabu ya Real Madrid ilielezwa kumuekea ofa ya mkataba wa mwaka mmoja mchezaji huyo kwani mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Lakini bado mchezaji huyo hajasaini kandarasi hiyo na taarifa zinaeleza huenda akabadili mawazo na kufata ofa nono katika nchi za Kiarabu.
Karim Benzema amekua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Real Madrid kwa muda mrefu akiitumikia kwa mafanikio makubwa, Lakini huu unaweza kua mwaka wa mwisho wa utumishi wake ndani ya mabingwa hao watetezi wa ulaya baada ya kipindi kirefu ndani ya timu hiyo.
Baada ya kuibuka kwa taarifa hizi inaelezwa kua klabu ya Real Madrid imeshaanza mchakato wa kuhakikisha wanapata mbadala sahihi wa Benzema sokoni, Huku miongoni mwa majina ambayo yanapewa kipaumbele zaidi ni jina la mshambuliaji wa klabu ya Tottenham raia wa kimataifa wa Uingereza Harry Kane.


