Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Eduardo Camavinga amefanikiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu ya Real Madrid mpaka mwaka 2029.
Eduardo Camavinga alikua bado ana mkataba ndani ya klabu ya Real Madrid lakini amefanikiwa kuongeza mkataba mwingine ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2029.Klabu ya Real Madrid imeweka kiasi cha Euro bilioni moja kwa klabu ambayo itahitaji saini ya mchezaji huyo, Hivo ni wazi klabu hiyo haifikirii kumuachia mchezaji huyo.
Real Madrid inawaongezea mikataba mirefu wachezaji wake wadogo kwa kile kinachoelezwa kutengeneza kizazi kipya kitakachodumu kwa muda mrefu zaidi ya timu hiyo kama ambavyo kizazi kilichopita kimefanya.Toni Kroos, Luca Modric, na wachezaji wengine wenye umri mkubwa wako mbioni kutimka klabuni hapo, Hivo Real Madrid imewaongezea mikataba wachezaji kama Federico Valverde, Camavinga, Rodrygo, Vinicius Jr, Tchouameni ambao wanatarajiwa kutengeneza kizazi kipya cha klabu hiyo na kuleta mataji klabuni hapo.