Camavinga Mbioni Kurejea

Kiungo wa klabu ya Real Madrid Eduardo Camavinga yuko mbioni kurejea kwenye kikosi hicho baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja na nusu baada ya kuumia mazoezini.

Camavinga alipata majeraha kuelekea mchezo wa Uefa Super Cup dhidi ya Atalanta ambapo aliumia goti lake na kumfanya nje ya uwanja kwa muda ambao amekaa, Lakini kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti amesema kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatarajiwa kurudi hivi karibuni.camavingaKocha huyo amesema “Atanza mazoezi na timu wiki ijayo.”

“Anajisikia vizuri. Ni muhimu sana kwa sababu tutaweza kufanya mzunguko wa viungo wa kati zaidi.”

Kiungo Camavinga anatarajiwa kurejea ndani ya klabu hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya mahasimu zao klabu ya Atletico Madrid kwa maana ya Madrid Derby, Kurejea kwa mchezaji huyo kutaisaidia timu hiyo kwa kiwango kkikubwa kwani timu hiyo imekua ikiandamwa na majeraha hivi karibuni haswa kwa wachezaji wao muhimu.

Acha ujumbe