Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Eduardo Camavinga ameondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kuelezwa kupata majeraha ya goti katika mazoezi.
Camavinga inaelezwa aligongana na mchezaji mwenzake Ousmane Dembele katika mazoezi jana na ndio imepelekea mchezaji huyo kupata majeraha ya goti.Kiungo huyo wa klabu ya Real Madrid inaelezwa atasafiri kurudi nchini Hispania kwajili ya kufanyiwa vipimo zaidi klabuni na timu ya madaktari ndani ya klabu ya Real Madrid.
Real Madrid imekua ikikumbwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu ikiwa na kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa atatakiwa awepo nje ya uwanja itaongeza idadi ya majeraha kwa wachezaji klabuni hapo, Lakini itakua ni pengo pia kwa klabu hiyo.Eduardo Camavinga amekua moja ya mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Real Madrid, Kwani amekua akitumika nafasi zaidi ya moja uwanjani, Hivo kukosekana kwake itakua ni pigo kwa klabu hiyo kuelekea michuano mbalimbali ambayo klabu hiyo inashiriki.