Mchezaji wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ureno Joao Cancelo anaelezwa anahitaji kutimkia klabu ya Fc Barcelona mabingwa wa soka nchini Hispania.
Joao Cancelo mpaka sasa inaelezwa ameshakubaliana maslahi binafsi na klabu ya Barcelona, Huku yeye mwenyewe akionekana kuhitaji kuondoka ndani ya klabu ya Man City ambapo anajiona kama sio sehemu ya mipango ya kocha Guardiola.Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez inaelezwa kalimuhitaji beki huyo wa kulia tangu dirisha dogo la mwezi Januari, Lakini alizidiwa kete na klabu ya Bayern Munich na mchezaji huyo akashindwa kujiunga na timu hiyo.
Mazungumzo bado yanaendelea baina ya vilabu viwili kati ya Barcelona na klabu ya Manchester City kwani upande wa mchezaji tayari ameshaonesha kila dalili ya kutaka kujiunga na klabu ya Barcelona.Barcelona wana mpango wa kutumia kiasi cha pesa ambacho watakipata kwa klabu ya PSG ambacho watamuuza mchezaji Ousmane Dembele ili kuhakikisha wanampata beki huyo wa kimataifa wa Ureno Joao Cancelo ambaye ni kipaumbele cha kocha Xavi.