Courtois Auaga Msimu Rasmi

Golikipa wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Ubelgiji Thibaut Courtois ameuaga msimu rasmi baada ya kupata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa miezi miwili.

Golikipa Courtois amepata jeraha tena ndani ya goti lake la kulia ambalo litamuweka nje ya uwanja kwa miezi miwili, Huku kimahesabu atakua ameuaga msimu kwani msimu unamalizika mwezi wa tano na majeraha ya golikipa huyo yatachukua miezi miwili ambapo ni kuanzia sasa mpaka mwezi wa tano.courtoisGolikipa huyo alipata majeraha ya goti mwanzoni mwa msimu huu ambapo yamemueka nje ya uwanja takribani miezi minne ambapo alifanyiwa upasuaji, Huku mpaka sasa alikua ameshaanza mazoezi na wenzake kabla ya kuumia tena.

Hii imekua taarifa mbaya na ya mshtuko kwa benchi la ufundi la klabu ya Real Madrid, Kwani golikipa huyo amekua nguzo ya klabu hiyo kwa muda mrefu akiibeba mara kadhaa na sasa anakwenda kukosekana kwa msimu wote uliobakia.courtoisGolikipa namba mbili ndani ya timu hiyo Lunin amekua na kiwango tangu kuumia kwa Courtois, Lakini bado wengi walitamani kumuona raia huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akirejea kwenye milingoti minne ya Real Madrid lakini hali imekua tofauti na ilivyotarajiwa.

Acha ujumbe