Mlinzi wa klabu YA Barcelona Dani Alves leo ametangaza rasmi kuachana na klabu hiyo kwa mara ya pili na hataongeza mkataba tena klabu hiyo baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa usajiri wa muda mfupi mwezi Janaury.

Dani Alves mwenye miaka 39 ameitumikia klabu ya Barcelona kwa vipindi viwili ambapo kipindi cha kwaza ni kuanzia mwaka 2008 hadi 2016, huku akiichezea klabu hiyo michezo 391 na kipindi cha pili akitumikia kwa miezi mitano tu na kuichezea michezo 17 tu na kukamilisha jumla ya michezo 408.

Dani Alves

“Ningependa kuwashukuru wafanyakazi wote kwa nafasi waliyonipa ili kurudi kwenye klabu hii, na kuweza kuvaa jezi ya klabu bora tena, hamjui ni kiasi gani nina furaha,” aliandika Dani Alves kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye kipindi chake akiwa na jezi ya Barcelona, amefanikiwa kushinda mataji sita ya La Liga, matatu ya ligi ya mabingwa na manne ya Copa del Rey.

Dani alves anatarajia kuwepo kwenye kikosi cha Brazili kitakachocheza komba la Dunia mwezi Novemba nchini Qatar, kwani ameshaitwa kwenye kikosi kilichocheza michezo ya kirafiki dhidi ya Japan na Korea Kusini na ameanza kwenye michezo hiyo.

Alves ni timu gani atakwenda ili kuichezea ili kupata nafasi ya kucheza kombe la dunia kwa mara ya mwisho mwaka huu?


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa