Beki wa kulia wa klabu ya Real Madrid, Dani Carvajal, anatarajiwa kuhitimisha safari yake ndani ya miamba hiyo ya Hispania mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20.
Kuondoka kwake kutafunga ukurasa muhimu katika historia ya Real Madrid kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa mmoja wa viongozi wa kikosi hicho kwa miaka mingi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Carvajal alijiunga na akademi ya Real Madrid mwaka 2002 akiwa na umri mdogo kabla ya kupanda hatua kwa hatua hadi kikosi cha kwanza. Alirejea rasmi kuitumikia timu hiyo mwaka 2013 akitokea klabu ya Bayer Leverkusen baada ya kuwa na msimu mzuri nchini Ujerumani. Tangu hapo, amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi ya Madrid.
Katika kipindi chake cha mafanikio ndani ya Santiago Bernabéu, Carvajal amecheza jumla ya mechi 450 na kufunga mabao 14 huku akisaidia timu hiyo kutwaa mataji 27 tofauti. Mafanikio hayo yanamweka miongoni mwa wachezaji wenye mataji mengi zaidi katika historia ya klabu hiyo, akifuata nyuma ya kiungo mkongwe Luka Modrić.
Miongoni mwa mataji aliyoyashinda ni pamoja na UEFA Champions League mara sita, La Liga mara nne, Copa del Rey mara mbili pamoja na mataji mengine ya kimataifa ikiwemo FIFA Club World Cup na UEFA Super Cup. Carvajal pia ameandika historia kwa kuwa mmoja wa wachezaji watano pekee waliowahi kushinda Champions League mara sita, huku akiwa mchezaji pekee aliyeanza katika fainali zote sita alizoshinda.
Mbali na mafanikio yake ngazi ya klabu, Carvajal pia ameendelea kung’ara akiwa na timu ya taifa ya Hispania ambapo ameichezea mechi 51. Ameisaidia Hispania kutwaa ubingwa wa UEFA Nations League pamoja na UEFA European Championship, jambo lililoimarisha zaidi nafasi yake kama mmoja wa mabeki bora wa kizazi chake katika soka la dunia.


