Ousmane Dembele anafuraha ndani ya Barcelona na anataka kusalia, huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha na kuhamia Paris Saint-Germain ya nchini kwao Ufaransa.

 

Dembele Atamani Kusalia Barcelona licha ya kuhusishwa na PSG

Dembele amekuwa na wakati mseto kwenye LaLiga tangu alipowasili Barca kwa pesa nyingi kutoka Borussia Dortmund mnamo 2017, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa na msimu mzuri tangu Xavi achukue usukani msimu uliopita.

Amehusika katika mabao mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote wa Blaugrana tangu Xavi alipokuwa kocha mkuu Novemba 2021, akifunga mabao nane na kutoa asisti 20.

Hiyo inajumuisha mabao sita na asisti saba katika mechi 22 msimu huu (michezo 17 imeanza), na Dembele pia alitoa pasi mbili za mabao katika mechi saba alizoichezea Ufaransa walipomaliza kama washindi wa pili kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar.

Dembele Atamani Kusalia Barcelona licha ya kuhusishwa na PSG

Hata hivyo, licha ya stori zinazodai kuwa PSG wanaweza kumleta kwenye Ligue 1, winga huyo wa zamani wa Rennes alikiambia kituo cha televisheni cha Eleven Sports cha Ubelgiji kwamba anaridhika Camp Nou.

“Nilisaini mkataba mpya Barca miezi minne iliyopita na nina furaha hapa, nataka kuendelea kufanya kazi na kuimarika Barcelona. Niko vizuri hapa, nina furaha Barcelona, ​​napenda maisha yangu hapa. Kocha ananiamini, na bodi inaniamini pia.”

Dembele amebakiza miezi 18 tu katika mkataba wake, lakini rais wa Barca Joan Laporta alisisitiza Alhamisi kwamba “hauzwi”, ikiwa PSG watakuja kumsajili, tutawaambia hauzwi.

Dembele Atamani Kusalia Barcelona licha ya kuhusishwa na PSG

Ni mmoja wa wachezaji muhimu sana tulionao. Ana kasi ya ajabu, ni mwanga wa radi. Kila anapopata mpira anasumbua ulinzi na juzi katika ushindi wa 4-3 wa Copa del Rey dhidi ya Intercity alifunga bao kubwa.

“Hataenda kwa euro milioni 70 au kiasi chochote.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa