Kinda wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 16 Endrick amesaini rasmi katika klabu ya Real Madrid kwa akitokea klabu ya Palmeiras ya nchini Brazil.

Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kumalizana na klabu ya Palmeiras na kumsajili mchezaji huyo kwa kiasi cha paundi milioni 72 na kinda huyo kusaini mkataba wa miaka nane mabingwa hao wa ulaya kuanzia 2022 mpaka mwaka 2030.endrickKlabu ya Real Madrid imeweka rekodi baada ya kumsajili mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 72 na kufanya kua mchezaji Endrick kua mchezaji ghali zaidi mdogo kuwahi kusajiliwa, Kwani mchezaji huyo ana miaka 16 kwasasa.

Kinda huyo kabla ya kujiunga na klabu ya Real Madrid alihitajika na vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya ikiwemo Barcelona, Manchester United, na Liverpool lakini mwisho ni klabu ya Real Madrid iliofanikiwa kunasa saini ya mchezaji huyo.endrickKinda Endrick ambaye atajiunga na klabu ya Real Madrid rasmi mwaka 2024 huku kwasasa akiendelea kusalia katika klabu yake ya Palmeiras, Huku mchezaji huyo akiahidi kuitumikia Palmeiras kwa kiwango kilekile mpaka pale ambapo ataondoka klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa