FC Barcelona Watangaza Kikosi cha Mchezo dhidi ya Deportivo Alavés.

FC Barcelona tayari wamehakikisha ubingwa wa La Liga kihesabu, lakini bado wana mechi tatu za kucheza kabla msimu wa ligi wa 2025-26 kumalizika rasmi. Katika michezo hiyo, Blaugrana watakuwa wakilenga kufikisha pointi 100.

FC Barcelona Watangaza Kikosi cha Mchezo dhidi ya Deportivo Alavés.

Mchezo wa kwanza kati ya hiyo unatarajiwa kuchezwa usiku wa leo, Jumatano, dhidi ya Deportivo Alavés katika uwanja wa Mendizorroza Stadium. Klabu hiyo ya Catalonia tayari imetangaza kikosi cha mchezo huo, huku kukiwa na baadhi ya mabadiliko kwenye orodha hiyo.

Beki Andreas Christensen amerejea kwenye kikosi baada ya kupona jeraha la muda mrefu lililomuweka nje tangu mwishoni mwa mwaka jana. Kwa upande mwingine, Fermín López na Frenkie de Jong wameachwa nje kwa sababu za kiufundi, huku Raphinha akisuspishwa kwa mchezo huo kutokana na kufikisha idadi ya kadi za njano.

Kikosi kamili kilichotangazwa na FC Barcelona ni kama ifuatavyo:

Makipa

  • Joan García
  • Wojciech Szczęsny
  • Eder Aller

Mabeki

  • Pau Cubarsí
  • Eric García
  • Alejandro Balde
  • Jules Koundé
  • Gerard Martín
  • João Cancelo
  • Ronald Araújo
  • Andreas Christensen
  • Xavi Espart
  • Álvaro Cortés

Viungo

  • Pedri
  • Gavi
  • Dani Olmo
  • Marc Bernal
  • Marc Casadó
  • Tommy Marques

Washambuliaji

  • Ferran Torres
  • Robert Lewandowski
  • Marcus Rashford
  • Roony Bardghji

Majeruhi

  • Lamine Yamal

Waliosimamishwa

  • Raphinha

Waliopewa mapumziko

  • Frenkie de Jong
  • Fermín López

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.