Frimpong Aikataa Barca

Beki wa kulia wa klabu ya Bayern Leverkusen mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Jeremie Frimpong amesema hajui kuhusu taarifa ambazo zinamuhusisha na kujiunga na miamba ya soka kutoka nchini Hispania klabu ya Barcelona.

Frimpong amekua akihusishwa na klabu ya Barcelona lakini beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi ameweka wazi kua yote yanayoendelea kumuhusu yeye ni tetesi na hakuna chochote cha kweli na sasa akili yake ameielekeza kwenye michuano ya Euro kuisaidia timu yake ya taifa.frimpongBeki huyo amekua na msimu mzuri sana ndani ya klabu ya Bayern Leverkusen chini ya kocha Xabi Alonso na kufanikiwa kutwaa mataji mawili, Lkaini beki huyo akiwa moja ya wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Leverkusen jambo ambalo limemfanya kutolewa macho na vilabu vingi vikubwa barani ulaya.

Beki huyo alifanikiwa kuhusika kwenye zaidi ya mabao 20 ya klabu ya Bayern Leverkusen msimu uliomalizika akishirikiana vyema na beki wa upande wa kushoto raia wa kimataifa wa Hispania Grimaldo, Beki Frimpong mbali na klabu ya Barcelona lakini pia anahusishwa na klabu ya Manchester United.

Acha ujumbe