Ligi kuu ya Hispania maarufu kama LALIGA, imezidi kuwa ya moto zaidi baada ya upinzani kuongezeka ambapo kwasasa Girona ameingilia kati wale Mahasimu wawili wakubwa klabuni hapo baada ya kuwa wa moto zaidi.

 

Girona Yazidi Kuuwasha Moto Yapaa Kileleni LALIGA

Girona amepaa kileleni hapo jana baada ya kumfunga Celta Vigo nyumbani kwake katika dakika za majeruhi kipindi cha pili na kufikisha pointi 28 mbele pointi tatu ya Real Madrid ambaye ana alama 25 kabla ya mchezo wake wa leo.


Bao hilo la ushindi lilitupiwa kimyani na Herrera katika dakika ya 90+1 ya mchezo ambao mwenyeji alimiliki mpira kwa asilimia kubwa sana.

Pia ikumbukwe kuwa timu hiyo mpaka sasa kwenye michezo yake 11 ambayo imecheza, imeshinda mechi 9 ikienda sare moja na kupoteza mchezo mmoja hadi sasa na kukusanya alama 28.

Girona Yazidi Kuuwasha Moto Yapaa Kileleni LALIGA

Huku Celta Vigo yenyewe ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi zake sita pekee baada ya kushinda mchezo mmoja, sare 3 na kupoteza mara saba. Hivyo timu hiyo bado ina kibarua kizito cha kufanya kabla mechi hazijachanganya.

 

 

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa