Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania Antoinne Griezmann ameweka wazi kua barani ulaya anataka klabu hiyo ndio iwe klabu yake ya mwisho kucheza.
Griezmann ameeleza kua anataka klabu ya Atletico Madrid ndio iwe timu yake ya mwisho kucheza barani ulaya baada ya hapo aende akafurahie maisha sehemu nyingine, Hii ikimaanisha kua mchezaji huyo hana mpango wa kucheza timu nyingine barani ulaya.Mchezaji huyo amesema yuko kiwango ambacho klabu hiyo inahitaji hivo yeye ataendelea kusalia klabuni hapo kwakua yeye pia anapenda kuwepo hapo, Kuhusu hatma yake amesema watu wasubiri kama klabu hiyo itaendelea kumpa nafasi.
Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa amesema kua klabu ya Atletico Madrid ina wachezaji wazuri wenye ubora, Hii ikionesha ni moja ya vitu vinavyomvutia kuendelea kubaki ndani ya viunga vya Wanda Metropolitano.Miezi kadhaa nyuma ilielezwa kua Antoinne Griezmann alikua akihitajika na vilabu kutoka Saudia Arabia, Lakini mchezaji huyo amesema ataendelea kusalia ndani ya Atletico lakini akiwa hajafunga milango kwa vilabu kutoka nje ya bara la ulaya hivo baada ya kuondoka Atletico anaweza kujiunga na vilabu hivo kutoka Saudia.