Kocha wa Barcelona, Hansi Flick ameripotiwa kuwa karibu kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuinoa klabu hiyo hadi mwaka 2028, baada ya kukubali masharti yaliyowekwa mezani na viongozi wa timu hiyo ya Hispania.
Kwa mujibu wa taarifa mkataba huo mpya pia utakuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi endapo pande zote zitakubaliana mwishoni mwa makubaliano hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Wakala wa Flick, Pini Zahavi, aliwasili mjini Barcelona jana kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya mkataba mpya wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 61.
“Hansi Flick ameonyesha nia ya kuendelea kubaki Barcelona na sasa kila kitu kiko katika hatua za mwisho za makubaliano,” ilieleza taarifa hiyo.

Flick ameendelea kung’ara tangu alipochukua nafasi ya Xavi Hernandez Mei mwaka 2024, ambapo aliiongoza Barcelona kutwaa mataji matatu ya ndani ya nchi katika msimu wake wa kwanza akiwa benchi.
Kwa sasa Barcelona ipo mbioni kutwaa ubingwa mwingine wa La Liga, ikihitaji alama moja pekee dhidi ya Real Madrid Jumapili ili kutangazwa mabingwa rasmi. Tayari Barca waliwahi kuwafunga Madrid mabao 3-2 katika fainali ya Spanish Super Cup mwezi Januari kupitia mabao ya Robert Lewandowski na Raphinha.


