Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard ameeleza hana mpango wa kuondoka klabuni hapo, Labda klabu hiyo imuhitaji yeye kuondoka lakini sio yeye kuhitaji kuondoka.

Kiungo huyo ameeleza hana mpango wa kuondoka klabuni hapo majira ya Januari kwasababu ana familia ndani ya Madrid pia analipenda jiji hili. Lakini ikitokea dirisha kubwa wakahitaji aondoke basi atakua hana namna.hazardStaa huyo ambaye amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara klabuni hapo tangu ajiunge mwaka 2018 jambo ambalo linamnyima nafasi ya kucheza kwa muda mrefu ndani ya timu hiyo mabingwa watetezi wa ulaya.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza kwasasa ana nafasi ya kuonesha ubora wake katika timu ya taifa ya Ubelgiji ambapo yeye ndio nahodha ndani ya timu hiyo licha ya kutokufanya vizuri ndani ya Real Madrid.hazardEden Hazard amekua akiwatia mashaka mashabiki wengi wa klabu ya Real Madrid tangu ajiunge klabuni hapo hajaonesha ubora ambao walioutarajia. Pamoja na kuandamwa na majeraha lakini mashabiki wamekua wakihoji juu ya uwezo wa nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji.


Mchezaji Hazard anasema ilikua ndoto yake toka akiwa kijana kuichezea klabu ya Real Madrid  na amesisitiza anahitaji kuitumikia klabu hiyo kwakua bado anajihisi mwenye deni mbele ya klabu na mashabiki wa klabu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa