Waswahili husema ‘kila chenye mwanzo, hakikosi kuwa na mwisho’. Kama ilivyokuzaliwa, kuna kufa. Javier Mascherano ametundika daruga kwenye ulimwengu wa soka la kulipwa.
Mashabiki na wadau wa mchezo wa soka wanafahamu ukubwa wa jina Javier Mascherano. Uwezo wake wa kuongoza safu ya ulinzi katika vilabu vikubwa kama Barcelona na Liverpool pamoja na timu ya taifa ya Argentina, utaendelea kukumbukwa daima.
Mascherano alitangaza kustaafu kucheza soka la kulipwa baada ya kuwa uwanjani kwa miaka 17.
Katika historia ya Argentina, Mascherano ndio mchezaji aliyecheza michezo mingi (147) akiwa na timu ya taifa hilo. Mwezi Januari, Mascherano aliamua kurudi nyumbani na kusajiliwa na timu ya Estudiantes de La Plata.
Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Argentinos Juniors kwa matokeo ya 1-0, Mascherano (miaka 36) alisema ni muda sahihi wa kuachana na soka.
“Ninataka kutangaza leo ninastaafu kucheza soka la kulipwa. Ninaishukuru klabu hii kwa kunipatia fursa ya kumaliza maisha yangu ya soka nikiwa Argentina.
“Niliitumikia taaluma yangu kwa 100% na nilifanya kila nililoweza. Leo nimegundua muda mwingine inakuwa ngumu kwangu na sitaki kuwavunjia heshima Estudiantes walioniamini na kunirudisha Argentina au wachezaji wenzangu au taaluma ya soka.” alisema Javier Mascherano.
Mascherano aliianza safari ya kucheza soka akiwa na klabu ya River Plate kabla ya kutimkia Corinthians kisha alijiunga na West Ham United na mwaka 2007 alisajiliwa na Liverpool.
2010 alijiunga na Barcelona ambapo alipata mafanikio makubwa zaidi alipokuwa Camp Nou. Alibeba mataji 5 ya LaLiga na 2 ya Ligi ya Mabingwa – UEFA kati ya mengine mengi.
Mascherano aliisaidia Argentina kufika fainali ya Kombe la Dunia 2014 ambapo walifungwa na Ujerumani kwenye dakika 30 za nyongeza. Walimaliza nafasi ya pili mara 4 kwenye Copa America na kubeba medali mbili za dhahabu kwenye Mashindano ya Olympic.
Baada ya kuitumikia Hebei China Fortune kwa miaka miwili, Javier Mascherano alirudi nyumbani na kujiunga na Estudiantes ambayo aliitumikia mpaka alivyotangaza kustaafu siku ya jana (Jumapili).
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.
magdalena
astaafu tu katumikia sana soka umri umeenda apumzike sasa
Elika
Bora apumzike tu
Carolyn
Mapumziko mema..
Fatina mfigi
Safi sana kazi na umri mapumziko mema
Rahma
Apumzike tu
Adelta
Mashabiki tunakutakiya Kila la kheri kwa kustafu
Ester jackson
Kila laheri kwenye maisha mampya
zeiyana
Hamafanya kazi kubwa kwenye ulimwengu wa soka javier historia yake haiwezi kufutika
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Sana umeitumia kazi yako kiufasaa kustafu kwako pongezi zako pumzika tuuu jembee
Angelina
All the best
Hopemwaikuka
Sio mbaya pumzka sasa
Mwajumah
Mapumziko mema
Sadick
Haina ubishi kwamba Jevier alijitoa mno kwa timu alizochezea na hata kauli yake ya kustaafu inadhirisha uaminifu wake
Povel
Javier pumzika kwa amani tutaenzi uhodari,kujituma,na mazuri yote ukifanya katika ulimwengu wa soka
Issa
Mpira kautendea haki javier masherano
Sabrina
Kazi na umri babu pumzika tu
aisha
Atakumbukwa sana jinsi alivyocheza soka
Sauda
Apumzike salama
Nasra
Bora iwe hvyo
Saupha mohamed
Bora apumzike
Tatu
Muda wake umefika awapishe na wengine tuone vipaji vyao nenda tu kapumzike