Winga wa klabu ya Atletico Madrid anayekipiga kwa mkopo ndani ya klabu ya Fc Barcelona Joao Felix inaelezwa mipango yake ni kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa uhamisho wa kudumu.
Rais wa klabu ya Atletico Madrid bwana Cerezo ameweka wazi kua Joao Felix anahitaji kuendelea kuitumikia klabu ya Barcelona kuliko kurudi Atletico na rais huyo bila kupepesa ameweka wazi mipango ya winga huyo.“Joao anataka kubaki Barcelona ni kawaida, Barcelona pia wanahitaji aendelee kubaki pale na yeye anahitaji pia, Ni mchezaji mzuri ameingia kwenye timu yao vizuri sijui Atletico watapata kiasi gani cha pesa wakati huu”
Winga huyo wa kimataifa wa Ureno ameonesha mara nyingi hataki kuendelea kucheza ndani ya klabu ya Atletico Madrid, Kwani alitolewa kwa mkopo klabu ya Chelsea lakini aliporudi klabuni hakutaka kuendelea alikubali kwenda tena kwa mkopo Barcelona ambapo ameeleza ndio klabu ya ndoto zake.Klabu ya Atletico Madrid ni wazi iko tayari kupokea ofa kutoka kwa klabu ya Barcelona kwajili ya winga wao Joao Felix, Kwani mchezaji huyo ameonesha wazi hana mpango wa kurejea ndani ya timu hiyo na anahitaji kuendelea kukipiga ndani ya klabu ya Barcelona.