Kiungo wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Marekani, Johnny Cardoso, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wa kulia baada ya kupata majeraha makubwa yaliyotikisa matumaini yake ya kushiriki Kombe la Dunia mwezi ujao.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Atletico Madrid, klabu hiyo ilieleza kuwa Cardoso alipata majeraha hayo wakati wa mazoezi yaliyofanyika Alhamisi iliyopita. “Cardoso alipata majeraha makubwa ya kifundo cha mguu yaliyoathiri sehemu ya kiungio na atalazimika kufanyiwa upasuaji,” ilieleza taarifa hiyo ya klabu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Majeraha hayo yanaongeza changamoto kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye msimu wake wa kwanza nchini Hispania umeendelea kukumbwa na matatizo ya kiafya. Cardoso pia alipata muda mchache wa kucheza katika dirisha la mechi za kimataifa mwezi Machi baada ya kucheza dakika 45 pekee kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji.
Kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, anatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya Kombe la Dunia mwishoni mwa mwezi huu. Hata hivyo, majeraha ya baadhi ya nyota wa kikosi hicho yanaendelea kuwa wasiwasi mkubwa kwa benchi la ufundi.
Nahodha wa timu hiyo Christian Pulisic pia amekosa baadhi ya michezo ya AC Milan kutokana na tatizo la misuli, huku Tim Weah na Tanner Tessmann nao wakikabiliwa na majeraha yaliyopelekea kukosekana uwanjani.
Marekani ambao ni wenyeji wenza wa Kombe la Dunia pamoja na Mexico na Canada, wanatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki dhidi ya taifa ya Senegal Mei 31 na timu ya taifa ya Ujerumani Juni 6 kabla ya kuanza rasmi kampeni yao ya Kundi D dhidi ya timu ya taifa ya Paraguay Juni 12 mjini Inglewood, California.


