Kwa mujibu wa gazeti la Hispania la Sport, Jose Mourinhoamedai kuondolewa kwa kocha wa mazoezi ya viungo raia wa Italia Antonio Pintus ikiwa atachukua kazi ya kuinoa Real Madrid.
Kumekuwa na ripoti nyingi katika siku chache zilizopita zikidai kuwa wachezaji wamekerwa na Álvaro Arbeloa na wanatafuta kocha mpya wa mbinu, huku wakifikiria pia uwezekano wa kurejea kwa José Mourinho.
Mourinho aliwahi kuichukua kazi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka Inter Milan kufuatia mafanikio yao ya Treble mwaka 2010, walipotwaa Serie A, UEFA Champions League na Coppa Italia.
Ili kurejea, inaripotiwa kuwa José Mourinho ana orodha ya masharti aliyoiweka wakati wa mazungumzo ya video na rais Florentino Pérez.
Masharti hayo yalijumuisha ombi la Real Madridkumfukuza kazi kocha wa mazoezi ya viungo raia wa Italia Antonio Pintus, mwenye umri wa miaka 63, ambaye amewahi kuwa na vipindi kadhaa klabuni hapo.
Pintus alijiunga na Madrid kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 2016 hadi 2019, kisha akaondoka kwenda kufanya kazi na Antonio Conte katika Inter Milan kuanzia 2019 hadi 2021.
Alirejea Real Madrid katika majira ya kiangazi hayo, akifanya kazi kama meneja wa utendaji na kocha wa mazoezi ya viungo katika majukumu mbalimbali.
Antonio Pintus pia amewahi kufanya kazi katika Juventus FC, Chelsea FC, Sunderland AFC, Olympique de Marseille na vilabu vingine.
Bado haijabainika ni kwa nini José Mourinho amesisitiza sana kutotaka Muitalia huyo awe sehemu ya benchi lake la ufundi.
Miongoni mwa masharti mengine, “The Special One” pia anataka mkataba wa angalau miaka miwili, klabu kumteua msemaji rasmi (jambo ambalo tayari alikuwa amekwisha lalamikia akiwa AS Roma), uhuru kamili katika maamuzi ya kiushindani (sporting decisions), na pia kuruhusu wachezaji kutafuta maoni ya pili ya kitabibu kuhusu majeraha yao.