Nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania ambaye yupo kwa mkopo klabuni hapo akitokea klabu ya Espanyol Joselu amesema anatamani kusalia ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji Joselu amesajiliwa kwa mkopo wa mwaka mmoja ndani ya Real Madrid akitokea klabu ya Espanyol, Huku kwenye mkataba wake kukiwa na kipengele cha kununuliwa jumla.Mshambuliaji huyo amepania kufanya makubwa katika kipindi hichi ambacho yupo kwa mkopo ndani ya Real Madrid kwajili ya kuishawishi klabu hiyo kumpa mkataba wa muda mrefu aweze kusalia ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.
Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Hispania mpaka sasa ameonekana kufanya vizuri ndani ya jezi ya Real Madrid, Kama ataendeleza kiwango anachokionesha sasa ndani ya timu hiyo ni wazi mabosi wa klabu hiyo wanaweza kumpa mkataba wa muda mrefu.Joselu kwasasa anaongoza safu ya ushambuliaji ya klabu ya Real Madrid sambamba na Vinicius Jr, Rodrygo, na kiungo mya wa klabu hiyo Jude Bellingham ambaye licha ya kua kiungo lakini amefanikiwa kufunga mabao kumi mpaka sasa.