Kipa wa klabu ya Chelsea ambaye anakipiga klabu ya Real Madrid kwa mkopo Kepa Arrizabalaga amesema anatamani kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo ambapo anakipiga kwa mkopo.
Golikipa huyo ambaye kwasasa yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Hispania ameweka wazi matamanio yake ya kuendelea kukipiga ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa muda wote barani ulaya.Kepa ameungana na mshambuliaji wa klabu hiyo Joselu ambaye na yeye jana aliweka wazi anatamani kuendelea kusalia ndani ya klabu ya Real Madrid kwakua yupo klabuni hapo kwa mkopo akitokea Espanyol.
Golikipa huyo amekua golikipa namba moja wa Real Madrid baada ya aliyekua golikipa namba moja wa klabu hiyo Thibaut Courtois kupata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda mrefu.Kepa Arrizabalaga amekiri kua hakuna mchezaji ambaye hatamani kuicheza klabu kama Real Madrid na kuweka wazi kua ana furaha kuendelea kuwepo klabuni hapo zaidi.