Refa raia wa kimataifa wa Hispania Antonio Mateu Lahoz ametangaza kustaafu kuchezesha soka mwishoni mwa msimu huu wa mwaka 2022/23.

Refa huyo ambaye amekua akishtumiwa na maamuzi yake ya kutatanisha katika michezo mbalimbali amesema kua anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu huu. Lahoz kwasasa amesimamishwa kuchezesha mchezo ligi kuu ya Hispania baada ya kutoa kadi nyingi katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania kati ya Espanyol dhidi ya Barcelona.lahozRefa Lahoz amekua akihudumu kwa muda mrefu katika ligi kuu ya soka nchini Hispania pamoja na michuano mikubwa barani Ulaya kama ligi ya mabingwa barani ulaya, Refa huyo pia amekua akichezesha michezo ya fainali ya kombe la dunia.

Refa huyo amekua akiibua utata mara kwa mara kutokana na maamuzi ambayo akiyatoa katika michezo ambayo amekua akiichezesha, Refa huyo ameingia kwenye vitabu vya historia kama miongoni mwa marefa ambao wamekua wakitoa kadi nyingi katika michezo ambayo akiisimamia.lahozRefa Lahoz ataikumbuka zaidi mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2021 kati ya Manchester City dhidi ya Chelsea ambapo refa huyo alikua mwamuzi wa mchezo, Hii itakua kumbukumbu kubwa sana kwake kwani ndio mchezo mkubwa zaidi refa huyo kuusimamia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa