Refa Antonio Mateu Lahoz hatakuepo kwenye michezo ya wikiendi hii baada ya kutoa kadi nyingi katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania kati ya Bracelona na Espanyol.

Refa Lahoz alipingwa vikali katika mchezo wa derby wikiendi iliyomalizika kati ya Espanyol dhidi ya klabu ya Fc Barcelona ambapo alitoa kadi mbili nyekundu kw wachezaji Jordi Alba na Vinicius Souza, Huku akitoa kadi zingine 11 za njano kwa wachezaji wengine.lahozRefa huyo aliingia kwenye matata jumatano tena kwenye mchezo wa Copa De le Rey baada ya kumpeleka jukwaani kocha wa Sevilla Jorge Sampaoli, Refa huyo amekua kwenye midomo ya watu kutokana na maamuzi yake ambayo amekua akiyafanya.

Refa Lahoz alipata shutuma hata kwenye michuano ya kombe la dunia haswa kwenye mchezo wa robo fainali kati ya Argentina na Uholanzi. Golikipa wa Argentina Emiliano Martinez alimshtumu refa huyo na kusema ni refa asiefaaa.lahozRefa huyo amekua akingia kwenye utata mara kwa mara kutokana na maamuzi ambayo amekua akiyachukua katika michezo tofauti tofauti, Vilevile amekua akipondwa kutokana na tabia yake ya kutoa kadi nyingi katika mchezo mmoja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa