Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema hawatafanya usajili katika dirisha dogo la mwezi Januari kutokana na sheria ya kifedha iliyowekwa na shirikisho la soka nchini Hispania.

Rais huyo amezungumzia shirikisho hilo wakati akiulizwa kuhusu kusajili mwezi Januari katika dirisha dogo na kuweka wazi kutokana na taratibu za kifedha zilizowekwa na La liga hawataweza kufanya usajili kwenye dirisha hilo.laportaKlabu ya Barcelona imekua kwenye matatizo ya kifedha kwa muda sasa hivo kuwafanya kulazimika kuwauza baadhi ya nyota wao kwasababu ya matatizo ya kifedha, Hata pale kwa gwiji Lionel Messi ambae alilazimika kuondoka klabuni hapo kwasababu za kifedha.

Rais Laporta amesema atajitahidi kuomba kwa shirikisho la soka nchini humo kuangalia namn ambayo wanaweza kuwasidia ili kuweza angalau kusajili wapate nafasi ya kusajili na kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.laportaBarcelona wameondokewa na beki wao mkongwe alietumika kwa mafanikio klabuni Gerard Pique ambae amestaafu siku kadhaa nyuma, Hivo ni wazi Barca watahitaji huruma ya shirikisho kulegeza sheria zao ila waweze kusajili lakini isipowezekana basi hawatasajili kama ambavyo rais Laporta ameeleza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa