Manchester United Wapo Tayari Kumuuza Marcus Rashford

Klabu ya Manchester United imeripotiwa kutokuwa na mpango wa kumrudisha mshambuliaji wake Marcus Rashford kikosini msimu ujao baada ya kumaliza kipindi chake cha mkopo katika klabu ya FC Barcelona.

Manchester United Wapo Tayari Kumuuza Marcus Rashford Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Manchester United uko tayari kumuachia nyota huyo kwa uhamisho wa moja kwa moja katika dirisha lijalo la usajili, huku ukiamini kuwa mustakabali wake haupo tena ndani ya Old Trafford licha ya mkataba wake kudumu hadi mwaka 2028.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Rashford mwenyewe anaripotiwa kuwa na hamu ya kuendelea kubaki Barcelona baada ya kuzoea mazingira ya klabu hiyo ya Hispania, lakini mabingwa hao wa zamani wa La Liga bado wanaonekana kusita kulipa ada inayotajwa kufikia pauni milioni 26 zinazohitajika kukamilisha usajili wake wa kudumu.

Manchester United Wapo Tayari Kumuuza Marcus Rashford Kutokana na hali hiyo, vigogo wengine wa Ulaya akiwemo Paris Saint-Germain pamoja na Arsenal FC wanaelezwa kuwa tayari kufuatilia kwa karibu maendeleo ya dili hilo huku wakipewa nafasi ya kuwasilisha ofa kubwa zaidi kwa mshambuliaji huyo wa England.

Manchester United Wapo Tayari Kumuuza Marcus Rashford Licha ya hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake, Rashford hivi karibuni aliipongeza Manchester United kwa kufuzu kucheza UEFA Champions League msimu ujao, lakini taarifa zinaonyesha wazi kuwa nyota huyo anaendelea kuonekana kuwa nje ya mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.