Mbappe Afunguka Kudhalilishwa Ndani ya Real Madrid

Nahodha wa France, Kylian Mbappe amesema kocha wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa amemuweka kama mshambuliaji wa nne katika kikosi hicho baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Oviedo.

Mbappe Afunguka Kudhalilishwa Ndani ya Real MadridMbappe aliingia kipindi cha pili dakika ya 68 baada ya Arbeloa kuanza na Vinicius Junior pamoja na Gonzalo Garcia katika safu ya ushambuliaji, huku nyota huyo wa Ufaransa akisisitiza kuwa alikuwa fiti kwa asilimia 100 kucheza tangu mwanzo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Nipo sawa kabisa. Sikuanza mchezo kwa sababu kwa kocha mimi ni mshambuliaji wa nne nyuma ya Franco Mastantuono, Vini na Gonzalo,” alisema Mbappe baada ya mchezo huo.

Mbappe Afunguka Kudhalilishwa Ndani ya Real MadridMchezaji huyo aliongeza kuwa hana tatizo lolote na Arbeloa licha ya maamuzi hayo ya benchi la ufundi. “Nilikuwa tayari kuanza, lakini ni uamuzi wa kocha na lazima uheshimiwe. Sina shida yoyote na Arbeloa, unatakiwa ukubali falsafa ya kocha na kufanya vizuri zaidi ili upate nafasi,” aliongeza.

Mbappe Afunguka Kudhalilishwa Ndani ya Real MadridMbappe pia amekuwa akikosolewa na baadhi ya mashabiki wa Real Madrid baada ya kusafiri kwenda Sardinia wakati akiendelea kuuguza majeraha ya misuli ya paja, ingawa alieleza kuwa safari hiyo ilikuwa imeidhinishwa rasmi na klabu.

Mbappe Afunguka Kudhalilishwa Ndani ya Real MadridKwa upande wake, Arbeloa alikanusha madai kuwa alimwambia Mbappe kuwa ni chaguo la nne katika ushambuliaji wa timu hiyo. “Nilizungumza naye kabla ya mchezo na sijui alitafsiri vipi mazungumzo yetu. Kwangu ilikuwa wazi kwamba mchezaji ambaye siku nne zilizopita hakuwa tayari hata kukaa benchi dhidi ya Barcelona hapaswi kuanza leo,” alisema kocha huyo huku akithibitisha kuwa Mbappe ataanza katika mchezo ujao dhidi ya Sevilla Jumapili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.