Kiungo wa klabu ya Real Maddrid na timu ya taifa ya Croatia Luca Modric amesema JudeBellingham hausiani na suala la yeye kuongeza mkataba ndani ya klabu ya Real Madrid.

Luca Modric kwasasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuongeza mkataba na klabu yake ya Real Madrid, Lakini wengi wakihisisha kuchelewa kuongeza mkataba kwa mchezaji huyo kunategemeana na kama Real Madrid itamsajili Jude Bellingham klabuni hapo basi yeye hataongeza mkataba jambo ambalo amelikanusha.modricKiungo wa klabu ya Borussia Dortmund Jude Bellingham anahusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid katika dirisha kubwa la usajili mwezi Juni, Huku kujiunga kwa mchezaji huyo ndani ya Real Madrid kukihusishwa kuzuia mkataba mpya wa Lukita klabuni hapo.

Luca Modric ambaye ameitumikia Real Madrid kwa zaidi ya misimu tisa mpaka sasa amesema anataka kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo zaidi, Huku mazungumo ya kuongeza mkataba baina ya mchezaji huyo na klabu yake yakiendelea na ikielezwa wapo kwenye hatua nzuri mpaka sasa.modricKocha wa wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua kiungo Luca Modric anastahili kuongozewa mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo, Hiyo kutokana na uwezo na ubora ambao anauonesha kila siku ndani ya timu hiyo tangu ameanza kuitumikia klabu hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa