Morata Kurejea Uwanjani Hivi Karibuni

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Alvaro Morata ametuma ujumbe kuoitia mitandao yake ya kijamii na kueleza kua majeraha ambayo aliyapata jana sio makubwa kama alivyodhani.

Morata jana alitoka uwanjani katika mchezo kati klabu yake ya Atletico Madrid dhidi ya Sevilla ambapo alipata jeraha la goti, Huku akishindwa kumaliza mchezo lakini ameweka wazi jeraha alilolipata sio kubwa sana hivo atarejea uwnajani hivi karibuni.morataMshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid amechukua fursa leo ya kuwashukuru mashabiki zake na wote ambao wamemtumia jumbe za kumpa moyo, Huku akisisitiza atakua sawa siku za hivi karibuni.

Mshambuliaji Alvaro Morata amekua na wakati mzuri tangu ajiunge na klabu ya Atletico Madrid akitokea klabu ya Juventus ya nchini Italia na kua moja ya wachezaji wanaofanya vizuri sana ndani ya klabu hiyo.

 

Acha ujumbe