Morata: Nilikaribia Kuondoka Atletico

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania Alvaro Morata amesema alikaribia kuondoka klabuni hapo katika dirisha kubwa la usajili lililopita.

Morata anasema alipata ofa mbalimbali kutoka katika vilabu mbalimbali nchini Saudia lakini aliamua kusalia ndani ya klabu ya Atletico, Huku sababu kubwa ikiwa kocha wake Diego Simeone.morataMshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid anasema anataka kushinda mataji na klabu hiyo, Kwani itakua furaha sana kushinda mataji na mabingwa hao wa zamani wa soka nchini Hispania.

Mshambuliaji huyo alisaini mkataba mara mbili ndani ya mwaka huu hiyo ni baada ya kukubali kusalia ndani ya klabu hiyo, Ambapo mshambuliaji huyo alikubali kuongeza mkataba mpaka 2026 na kuongeza mwaka mwingine mmoja.morataAlvaro Morata amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Atletico Madrid na kumfanya kocha wa klabu hiyo kutotaka mshambuliaji huyo kuondoka klabuni hapo kutokana na ubora ambao anaonesha siku baada ya siku.

Acha ujumbe