Nacho Kuendelea Kukipiga Ndani ya Madrid

Beki wa klabu ya Real Madrid raia wa kimataifa wa Hispania Nacho Fernandez ataendelea kukipiga ndani ya klabu hiyo baada ya kukubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo.

Nacho wakati anazungumza na waandishi amesema amepata ofa nyingi kutoka nje ya klabu ya Real Madrid lakini ameamua kusalia ndani ya timu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja, Beki huyo atasaini mkataba mpya wiki ijayo ambao utamuweka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2024 mwezi Juni.NachoBeki huyo alikua akihitajika na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia lakini ameweka wazi ana furaha kuendelea kusalia ndani ya Real Madrid na ndio sababu ameamua kuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi ili kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.

Nacho Fernandez ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wameitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu mpaka na wanaendelea kuichezea Real Madrid, Kwani mchezaji huyo ameanza kuitumikia timu ya wakubwa mwaka 2011.NachoBeki Nacho pia ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wameshinda mataji mengi ndani ya timu hiyo mpaka sasa akifanikiwa kushinda kila taji klabuni hapo na amekua mchezaji muhimu pale ambapo anahitajika na mwalimu.

Acha ujumbe