Pau Torres: Mambo Mazuri Yatakuja

Akiwa anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United, Pau Torres amebainisha kuwa mambo mazuri yapo njiani, kwa sasa kuna utulivu tu!

Kwa mujibu wa nyota huyu, ambaye hana uhakika juu ya hatma yakje kuelekea msimu mpya, ni kwamba ana mpango wa kuuanza msimu mpya wa 2021-22 akiwa na Villarreal.

Staa huyu wa miaka 24 alifanya vyema akiwa na Villarreal msimu uliopita, na amejikuta akiwa kwenye rada za vilabu vya Manchester United na Real Madrid katika dirisha hili la uhamisho la msimu wa joto.

Pau Torres Villarreal

Hata hivyo, Torres kwa sasa yupo katika majukumu ya kitaifa na timu yake ya taifa ya Hispania kwenye Euro 2020, na ameweka wazi kuwa bado anafurahia kuendelea kuwepo Villarreal, na angependa kuanza msimu ujao na mabingwa hao wa Ligi ya Europa.

“Kwa sasa ninazingatia kibarua cha Euro. Kisha nitageukia Super Cup na mambo mazuri yatakuja, hivyo nina utulivu kabisa.”

 

“Ninaishi kwenye mji wangu wa nyumbani, kuna ukimya, nafanya vitu vizuri na kupambania mambo makubwa nikiwa na timu ya mji wangu wa nyumbani. Nina utulivu wa hali ya juu hapa.”

 

– Pau Torres

Torres amecheza mechi 87 kwa timu yake ya sasa tangia alipojiunga nao kwa £50m kutoka Arsenal.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe