Rais wa klabu ya Real Madrid CF, Florentino Pérez, ameongeza tetesi za uhamisho wa mshambuliaji wa Manchester City FC, Erling Haaland, kuelekea Santiago Bernabéu, licha ya mchezaji huyo kuwa amesaini mkataba mrefu wa kuendelea kubaki klabuni hadi mwaka 2034.
Haaland amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu, akiwa ameifungia Manchester City mabao 37 na kutoa pasi za mabao nane katika mechi 50, hali inayoendelea kuongeza uvumi wa klabu kubwa kumuwania huduma yake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza na LaSexta, Pérez alikwepa kutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu Haaland lakini alisisitiza historia ya Real Madrid kusajili wachezaji bora duniani.
“Bila shaka. Tumekuwa tukifanya usajili kila mara; tumekuwa tukisajili wachezaji bora. Nimesajili Figo, Kaká, Ronaldo ‘The Phenomenon’, Beckham… akiwa mchezaji mzuri, namfuata,” alisema Pérez.
Alipoulizwa moja kwa moja kuhusu Haaland, alijibu “Haaland? Sitoi maoni kuhusu hilo. Hilo ni jukumu la idara ya usajili; mimi siingilii masuala ya kiufundi ya michezo.”
Tangu ajiunge na Manchester City akitokea Borussia Dortmund mwaka 2022, Haaland amefunga mabao 161 na kutoa pasi 29 za mabao katika mechi 196, akijidhihirisha kama mmoja wa washambuliaji hatari zaidi duniani.


