Perez : Rodri Hakustahili Ballon D'or

Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez ameongea kauli ambayo imeakisi kabisa kua kiungo wa klabu ya Manchester City Rodri hakustahili tuzo ya Ballon D’or mbele ya mchezaji Vinicius Jr.

Florentino Perez ameeleza kua Rodri ni mchezaji mzuri kweli hilo halina shaka lakini kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa msimu uliopita mbele ya Vinicius Jr sio jambo ambalo Rais huyo wa Real Madrid ameonesha kukubaliana nalo ambapo anaamini kuna hujuma ilifanyika mchezaji wake asishinde tuzo.Perez“Ballon d’Or? Bila shaka Rodri ni mchezaji bora wa soka, na anatoka Madrid, tunampenda sana. Alistahili Ballon d’Or… lakini si mwaka huu, mwaka uliopita.”

“Hii ilikuwa ni kwa mchezaji wa Real Madrid.

Halikadhalika baada ya kuzungumza hayo Perez alituma ujumbe kwa mchezaji wake Vinicius Jr akimueleza kua yeye ni mchezaji bora duniani “Vinicius, wewe ndiye mchezaji bora duniani.”

“Nataka ujue kwamba mashabiki wa Real Madrid wanajivunia wewe, kwa kila kitu ulichovumilia katika nyakati nyingi zisizo za haki. Yote haya yamekufanya kuwa mchezaji uliyo leo.”

Acha ujumbe