Mchezaji wa FC Barcelona Gerad Pique ametangaza kustaafu soka katika umri wa miaka 35 baada ya kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu na kwa mafanikio zaidi, huku kustaafu kwake kunaweka historia kubwa kwenye klabu hiyo.

 

Pique Atangaza Kustaafu Soka

Pique alishinda mataji nane ya Laliga, Ligi ya Mabingwa mara tatu akiwa na Barca huku akiisaidia timu yake ya Taifa kubeba Kombe lao la kwanza la Dunia mwaka 2010 na Ubingwa wa Ulaya miaka miwili baadae.

Beki huyo wa kati ameamua kustaafu soka na atacheza mechi yake ya mwisho hapo Jumamosi ambapo Barca watakuwa wakimenyana dhidi ya Almeria baada ya kuichezea klabu yake ya nyumbani zaidi ya mechi 600.

Pique anastaafu akiwa kama Gwiji wa Camp Nou, akiwa na wachezaji wanne pekee waliochezea Barcelona mara nyingi zaidi yake, ambao ni Lionel Messi (778), Xavi (767), Sergio Busquets (694) na Andres Iniesta (674) na wote walisaidia kuunda timu kubwa ya Barca katika miaka ya 2010 pamoja na Pique.

Pique Atangaza Kustaafu Soka

Mchezaji huyo alianza katika safu ya vijana ya Barca lakini aliondoka kwenda Manchester United mnamo 2004, ambapo alishinda Ligi ya Primia Ligi na Ligi ya Mabingwa msimu wa 2007-08. Na baadae alirejea Barca mwaka 2008 na ameshinda michezo 422 kati ya 614 katika mashindano yote tangu wakati huo.

Alinyanyua mataji 30 akiwa na klabu hiyo katika kipindi ambacho kilikuwa cha mafanikio zaidi katika historia ya Barca, pia aliweka alama yake katika kiwango cha Kimataifa, akiichezea Uhispania mara 102 kati ya 2009 na 2018.

Ni Sergio Ramos (135) pekee aliyecheza mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa kama mlinzi kuliko Pique ambaye amecheza michezo (128), huku akifunga mabao mengi zaidi kwa mlinzi kwenye kinyang’anyiro hicho na Roberto Carlos (16).

Pique Atangaza Kustaafu Soka

Msimu wake bora zaidi wa Ligi ya Mabingwa ulikuwa msimu wa 2008-09 alipomaliza akiwa na mipira mingi zaidi (90), huku ni Xavi (967) pekee aliyemaliza pasi nyingi zaidi yake (695).

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa