Aliekua beki wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ambae amestaafu hivi karibuni Gerard pique amezungumzia juu ya suala la yeye kuja kua rais wa klabu hiyo siku zijazo.

Beki huyo ambae aliagwa katika dimba la Camp Nou wikiendi iliyopita, ameweka wazi azma yake ya kuja kuiongoza klabu hiyo ya maisha yake ambayo ameitumikia kwa takribani miaka 14 kabla ya kuamua kustaafu.piquePique ameondoka ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kuitumikia kwa miaka 14 na kuisaidia kushinda kila taji kwenye ngazi ya klabu ikiwemo La liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya,Spanish super Cup pamoja klabu bingwa ya dunia ikiwa ni baadhi ya mataji ambayo amebeba klabuni hapo.

Beki huyo anafikiria kuja kuiongoza klabu hiyo siku moja lakini kwasasa atafanya mambo mengine baada ya kustaafu na hiyo inaweza kua siku za baadae.piqueBeki Pique pia amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United na kufanikiwa kubeba mataji ya ligi kuu ya Uingereza mawili pamoja na ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2008.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa