Mshambuliaji wa FC Barcelona, Marcus Rashford, ameandika historia mpya katika mchezo wa El Clasico baada ya kufunga bao la moja kwa moja la mpira wa adhabu dhidi ya Real Madrid kwenye ushindi wa mabao 2-0 uliochezwa Camp Nou Jumapili usiku.
Rashford aliifungia Barcelona bao la kuongoza dakika ya tisa kwa shuti kali la free-kick lililoelekea kona ya juu kushoto ya lango, huku kipa Thibaut Courtois akishindwa kabisa kuuzuia mpira huo uliowapa wenyeji mwanzo mzuri wa mchezo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa bao hilo, Rashford amekuwa mchezaji wa kwanza wa Barcelona kufunga moja kwa moja kupitia mpira wa adhabu katika El Clasico tangu Lionel Messi alipofanya hivyo mwezi Oktoba mwaka 2012. Rekodi hiyo ilikuwa imedumu kwa miaka 14 bila mchezaji wa Barcelona kufanikiwa kuifunga Real Madrid kwa namna hiyo.
Barcelona waliendelea kuutawala mchezo huo na kuongeza bao la pili dakika ya 18 kupitia Ferran Torres, aliyemalizia vizuri shambulizi la haraka na kuwakaribisha zaidi Blaugrana kwenye ubingwa wao wa 29 wa LaLiga.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Rashford alisema “Ni hisia za kipekee kufunga katika El Clasico, hasa kwa free-kick. Mashabiki walikuwa wa ajabu na ushindi huu ni muhimu sana kwa timu.” Bao hilo lilikuwa la nane kwa mshambuliaji huyo katika msimu wa 2025/26.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa amefunga mara ya mwisho katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Getafe CF, na kiwango chake kizuri kimeendelea kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Barcelona chini ya kocha Hansi Flick msimu huu.


