Klabu ya Real Madrid inamuwinda beki wa kimataifa wa Canada anayekipiga klabu ya Fc Bayern Munich mabingwa wa soka nchini Ujerumani Alphonso Davies.

Real Madrid wanamuwinda beki Alphonso Davies ambaye wanahitaji aje kuziba pengo la Ferlan Mendy ambaye anaonekana hajaweza kuonesha kiwango bora sana kwenye nafasi hiyo, Lakini vilevile beki Mendu amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara.Real MadridBayern Munich wanaelezwa kuhofia kua Madrid wanaweza wakafanikiwa kumshawishi mchezaji kujiunga na klabu hiyo, Hivo wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanambakiza au kutafuta mbadala wake haraka iwezekanavyo.

Real Madrid msimu uliomalizika imekua haina beki wa kushoto asili mara nyingi kwani beki Ferlan Mendy amekua akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara jambo ambalo limewafanya klabu hiyo kumuhitaji Davies kutoka Bayern Munich.Real MadridAlphonso Davies mwenye umri wa miaka 22 tu amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya klabu ya Bayern Munich tangu alipopata nafasi ndani ya timu hiyo mwaka 2019, Kitu ambacho kimewavutia Real Madrid ni mwendelezo wa kiwango bora kwa beki huyo kutoka Canada.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa