Real Madrid Wambeba Guler Mbele ya Barca

Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kuipiku klabu ya Barcelona kwa kinda wa kimataifa wa Uturuki anaefanya vizuri kwasasa ndani ya klabu ya Fenerbahce Arda Guler.

Real Madrid walikua wanamuwania Arda Guler ambaye pia alikua anawania wa na wapinzani wa klabu hiyo klabu ya Barcelona, Lakini taarifa zinaeleza kua mchezaji huyo mpaka sasa uelekeo wake ni kwa klabu ya Madrid mabingwa wa muda wote wa ulaya.Real MadridArda Guler amekua kwenye kiwango bora kabisa ndani ya Fenerbahce na kutabiriwa makubwa siku za usoni jambo ambalo lilifanya vigogo hao wa soka kutoka nchini Hispania kuingia vitani kwajili ya kunasa saini ya kinda huyo fundi.

Real Madrid wapo kwenye hatua za mwisho katika kuhakikisha wanamsajili Arda Guler kwani mpaka Rais wa klabu ya Fenerbahce Ali Koc amethibitisha kua kinda huyo anaondoka klabuni hapo japo walipambana kuhakikisha wanampata mchezaji huyo.Real MadridMabingwa wa muda wote wa ulaya klabu ya Real Madrid wamekua wakifanya usajili wa vijana wadogo wenye vipaji, Kwani wanahitaji kutengeneza timu tishio ya muda mrefu na mpaka sasa wameshasajili wachezaji wenye umri mdogo kwani hata Arda Guler ana umri wa miaka 18 tu.

Acha ujumbe