Real Madrid Hawatasajili Januari

Klabu ya Real Madrid hawana mpango wa kusajili mchezaji yeyote katika dirisha dogo la mwezi Januari, Hili limethibitishwa na kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti leo akiongea na waandishi wa habari.

Kocha Ancelotti ameweka wazi Real Madrid haina mpango wa kuingia sokoni katika dirisha dogo la mwezi huu, Hii inadhihirisha kua klabu hiyo imejitosheleza na inaridhidhwa na wachezaji waliopo klabuni hapo.real madridTaarifa zilikua zinaeleza kua klabu hiyo itaingia sokoni kusajili beki wa katikati kutokana na mabeki wa kati wa klabu hiyo kupata majeraha akiwemo David Alaba na Eder Millitao, Lakini kocha Ancelotti amekanusha na kusema mpango wa kusajili mchezaji yeyote Januari hii haupo.

Kocha huyo alisisitiza kwenye kesi ya beki wa katikati na kusema yupo Rudiger, Nacho, kiungo Tchouameni ambaye anatumika kwenye nafasi hiyo kwasasa, Lakini pia bila kumsahau beki Dani Carvajal ambaye kocha huyo amesema ana uwezo wa kucheza beki wa kati.real madridReal Madrid imekua ikiandamwa na majeraha mara kwa mara hasa kwa wachezaji muhimu, Hivo ilifikiriwa wataingia sokoni kwenye dirisha dogo mwezi huu kwajili ya kuboresha kikosi chao, Lakini taarifa za kushangaza ni kua mabingwa hao wa muda wote barani ulaya hawatafanya usajili wa aina yeyote.

 

Acha ujumbe