Real Madrid Kuwapata Militao, na Courtois Karibuni

Klabu ya Real Madrid inatarajia kua na wachezaji wake wawili muhimu hivi karibuni ambao wamekua wamekua nje ya kikosi kwa muda mrefu kwasasa ambao ni Eder Militao, na golikipa Thibaut Courtois.

Beki Eder Militao pamoja na kipa Thibaut Courtois wamekua nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu mpaka minne, Jambo ambalo limeifanya Real Madrid kuyumba kidogo haswa katika safu yao ya ulinzi.real madridBaada ya sare ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya jana usiku dhidi ya Rb Leipzig na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali, Ndipo kocha Carlo Ancelotti alipoweka wazi kua anatarajia kua na wachezaji wake katika hatua ya robo fainali.

Wachezaji hao wawili wakirejea kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya itaweza kuimarisha kikosi hicho, Kwani siku za hivi karibuni klabu hiyo imekua kwenye ikipata wakati mgumu kwenye safu ya ulinzi mpaka kufikia hatua ya kumchezesha kiungo Tchouameni kwenye eneo la ulinzi.real madridHii imekua taarifa njema kwa benchi la ufundi wa la Real Madrid kutokana na klabu hiyo kupitia kipindi kigumu kwenye safu yao ya ulinzi, Hivo kurejea kwa Militao na Courtois kutaimarisha safu ya ulinzi ya klabu hiyo ambayo ilionekana kua kwenye wakati mgumu.

Acha ujumbe