Real Madrid Kumpa Mkataba Mpya Lunin

Klabu ya Real Madrid inapanga kumpa mkataba mpya golikipa wake namba mbili raia wa kimataifa wa Ukraine Andriy Lunin ambaye kwasasa anafanya vizuri kwasasa klabuni hapo.

Golikipa wa huyo wa kimataifa wa Ukraine ndio amekua chaguo la kwanza klabuni hapo kwasasa kutokana na golikipa Thibaut Courtois ambaye amepata majeraha klabuni hapo na atakosekana msimu huu wote.luninMkataba wa sasa wa golikipa Lunin unamalizika mwezi Juni mwaka 2025 ina maana golikipa huyo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu, Jambo ambalo limewafanya Madrid kuanza mazungumzo ya mkataba mpya.

Uongozi wa klabu ya Real Madrid unaelezwa kua una imani na golikipa Lunin na suala la kusaini mkataba limebaki kwa golikipa huyo kwani upande wa klabu wako tayari wakati wowote kumpa mkataba asaini ili aendelee kua sehemu ya mabingwa hao wa muda wote barani ulaya.luninGolikipa huyo ameonesha ubora mkubwa kipindi hichi ambacho golikipa Thibaut Courtois amepata majeraha makubwa, Hivo Real Madrid wamefurahishwa na kiwango ambacho kimeoneshwa na Lunin na kuamua kumpa mkataba mpya.

Acha ujumbe