Klabu ya Real Madrid kutoka nchini Hispania imeshinda vita ya kumsajili kijana mdogo Endrick mwenye ubora mkubwa kutoka nchini Brazil mwenye umri wa miaka 16 kutoka klabu ya Palmeiras.
Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kumnasa kinda Endrick ambaye alikua anawaniwa na vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya kama klabu ya PSG.Lakini vigogo hao wa soka barani ulaya wamefanikiwa kushinda vita hiyo na kumsajili kinda huyo mwenye kipaji kikubwa kutok nchini Brazil.Mabigwa hao wa ulaya wamekubaliana na klabu ya Palmeiras kwa dau la paundi milioni 60 kumnyakua kinda huyo aliyezaliwa mwaka 2006 na kuvunja rekodi ya usajili baada ya kutoa kiasi hicho cha pesa kwa mchezaji mdogo kama Endrick.
Endrick amefanikiwa kuteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni baada ya kuhitajika na vilabu vikubwa barani ulaya kutokana kipaji chake cha ajabu licha ya umri wake kua mdogo,Lakini ameonesha uwezo mkubwa sana ndani ya klabu ya Palmeiras inayoshiriki ligi kuu nchini Brazil maarufu kama Serie A.Klabu ya Real Madrid inafanikiwa kupata saini ya wachezaji wadogo wenye vipaji kutoka nchini Brazil kwa miaka ya hivi karibuni, Hiyo ni baada ya kupata saini ya wachezaji kama Vinicius Jr na Rodrygo Goes ambao wanafanya makubwa ndani ya klabu hiyo kwasasa.